Ushindi wa bao 1-0 ambao kinadada wa Simba Queens wameupata dhidi ya Baobab Queens, umewahakikishia kutetea ubingwa wao kwa msimu wa pili mfululizo
Wababe hao wa soka la Wanawake, wamefikisha alama 54 wakiwaacha nyuma watani zao Yanga Princess wakiwa na alama zao 53
Kocha Mkuu wa Simba Queens Mussa Hassan Mgosi aliahidi kuubakisha ubingwa Msimbazi, amefanya hivyo kwa mara ya pili
Kuna watu waliwekeza nguvu kubwa kwenye mechi za kukamilisha msimu leo hasa baada ya kuona huko kwa Wanaume hawana chao
Lakini kinadada wa Simba Queens ni mabingwa na hawakuwa na presha yoyote licha ya kuchelewa kujipatia bao lao la ushindi dhidi ya Baobab Queens
Msimu huu kama uliopita tu, makombe yote yanarudi Msimbazi, hakuna namna...!
ADVERTISE HERE