Tutajipanga tufanye vizuri nyumbani - Gomes

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 May 2021
Tutajipanga tufanye vizuri nyumbani - Gomes

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema matokeo waliyopata Afrika Kusini kwa kufungwa mabao 4-0 na Kaizer Chiefs yamechangiwa na makosa waliyofanya katika mchezo huo

Kukosekana kwa umakini katika eneo la ulinzi na washambuliaji kutotumia nafasi, ni miongoni mwa sababu zilizopelekea Simba ipoteze mchezo huo kwa idadi kubwa ya mabao

Gomes amesisitiza mchezo huo bado haujamalizika, wana dakika nyingine 90 nyumbani, lolote linaweza kutokea

"Tulijua mchezo utakuwa mgumu sana, mpira wa miguuΒ  ni mchezo wa makosa, tumefanya makosa tumeadhibiwa.Β  Pia hatukuwa na matumizi mazuri ya nafasi. Tumepoteza kwa kufungwa magoli mengi, tutajipanga tuangalie nini kitatokea nyumbani kwa kuwa mchezo wa mpira una miujuza muda mwingine," alisema Gomes

"Jambo lolote linawezekana kwenye mpira, hatujafurahia matokeo lakini bado tuna matumaini, ni muhimu sana kuamini kwamba tunaweza kubadili matokeo. Lakini kama tunataka kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudiano lazima tuwe bora zaidi."

Pamoja na Simba kumiliki mpira kwa zaidi ya asilimia 65, Kaizer Chiefs walikuwa bora sana kwenye ulinzi na hatari katika mashambulizi yao ya kushitukiza kupitia winga zao

Aidha kocha Gomes ana kazi ya kufanya kwenye safu yake ya ulinzi hasa katika kucheza mipira ya krosi zinazotokea pembeni

Mabao matatu waliyofunga Chiefs yalitokana na mpira ya krosi, Simba inafungwa mabao mengi ya aina hiyo hata hapa nyumbani

Kaizer Chiefs walipata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa mlinzi Mathoho Erick kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Bernard Parker.

Mserbia Nurkovic akaongeza la pili kwa kichwa dakika ya 33 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Manyama Lebogang.

Bao la tatu likawekwa kambani tena na Nurkovic dakika ya 57 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya mpira uliookolewa na Mohamed Hussein kuanguka katika eneo hatari

Castro akaongeza la nne kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Manyama kutoka upande wa kulia

Mipira hii ya krosi ni shida kubwa sana kwa safu ya ulinzi ya Simba, kocha Gomes anapaswa kutatua changamoto hii ili kuhakikisha Chiefs hawafungi bao lolote katika mchezo wa marudiano ambao Simba itahitaji kufunga mabao matano

Kwani kama Chiefs watafunga bao Dar, Simba italazimika kupata ushindi wa kuanzia mabao sita

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’