Kiungo Mo aomba radhi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Mar 2018
Kiungo Mo aomba radhi Simba
Kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim "Mo" ameiomba radhi klabu yake kutokana na tabia ya utovu wa nidhamu ambao ameuonyesha na kusababisha kuwa nje ya kikosi kinachombana kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika, imeelezwa.

Hatua hiyo ya Mo, imekuja siku chache baada ya Kocha Mkuu wa Simba Mfaransa, Pierre Lechantre kusema kuwa kiungo huyo amekuwa akishindwa kuweka kipaumbele programu ya mazoezi na mara kwa mara akiomba ruhusa kwa sababu ambazo ameziita si za msingi.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah "Try Again" alisema kuwa uongozi wa klabu hiyo ulikutana na mchezaji huyo na baada ya kikao, nyota huyo aliyesajiliwa akitokea Mtibwa Sugar, aliandika barua ya kuomba radhi na kuahidi hatarudia makosa aliyokuwa anafanya.

Salim alisema kikao hicho kilizaa matunda na wanaamini kitamsaidia kurejea katika "mstari" na tayari kila mchezaji ameelezwa kuwa hakuna ambaye yuko juu ya timu.

"Sipendi kuweka wazi kila kitu kilichozungumzwa katika kikao hicho, lakini kwa kifupi Mo ameahidi kujirekebisha na kurejea kwenye hali yake ya kawaida," alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa Simba ina kanuni na sheria zake, hivyo mchezaji anapokosea, anaadhibiwa kwa kufuata misingi hiyo iliyowekwa na ni yenye lengo la kuhakikisha nidhamu inaimarika
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
28m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’