Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amesema hawakutegemea kupoteza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs kwa idadi kubwa ya mabao
Simba imefungwa mabao 4-0 katika mchezo ambao mabingwa hao wa Tanzania walipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri
Manara amesema timu haikucheza vizuri leo, makosa mengi yalifanyika, hata hivyo amesema Simba bado ina nafasi ya kurekebisha makosa hayo kwenye mchezo wa marudiano
"Tumefungwa na aliye bora usiku wa leo,tumecheza hovyo na tumefanya makosa mengi yaliyostahili adhabu hii"
"Maisha yanaendelea bado tunazo dakika tisini nyingine za kuamua,"Β amesema Manara
Nae Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema wamekubali kupoteza mchezo leo lakini wanayo nafasi ya kulipa kisasi nyumbani
"Timu bora imetufunga. Bado tuna dakika 90 kwa Mkapa. Naomba tuvute subira, kama walishinda 4 kwao, na sisi tunaweza kupindua nyumbani Insha'Allah. Mpira hautabiriki. Tujiamini. Tutaonana wiki ijao"
Mchezo wa marudiano utapigwa wiki ijayo, May 22 katika uwanja wa Benjemin Mkapa