Ndicho unachoweza kusema baada ya kushuhudia Simba ikifungwa mabao 4-0 na Kaizer Chiefs katika mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika, mkondo wa kwanza
Matokeo ya mchezo huu ni kinyume na matarajio ya wengi, wakati mwingine ndivyo mpira wa miguu ulivyo
Pamoja na kumiliki mpira kwa muda mwingi, Kaizer Chiefs walikuwa bora sana kwenye mashambulizi yao ya kushitukiza
Makosa katika safu ya ulinzi, yameigharimu Simba leo Chiefs wakifunga mabao matatu kupitia mipira ya vichwa
Safu ya ulinzi leo imefanya makosa mengi, Chiefs wametumia makosa hayo kujipatia ushindi mnono
Simba sasa inahitaji kujipanga ili kuhakikisha wanashinda angalau mabao matano kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es salaam wiki ijayo
Ni siku mbaya ofisini....!