Saa moja usiku Tanzania na Afrika Mashariki itaelekeza macho kwenye runinga zao kuwashuhudia mabingwa na wawakilishi wetu Simba katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs
Ni nadra sana kwa timu zetu za ukanda huu wa Afrika Mashariki kupata mafanikio kwenye michuano mikubwa barani Afrika ngazi ya vilabu, Simba imekuwa mwakilishi mzuri
Mechi hii dhidi ya Kaizer Chiefs itatizamwa na mashabiki wengi sana Afrika Mashariki kwani itarushwa mbashara na vituo mbalimbali vya runinga katika ukanda huu
Hapa nchini ZBC 2 watakuwa mbashara wakati kule Kenya KBC 1 ambayo ni runinga ya Taifa, imethibitisha watakuwa mbashara
Mchezo huo pia utaonekana kule Rwanda, Burundi na Uganda
Naamini nchi zote hizi mashabiki wataiunga mkono Simba kwani ushindi wao utaitangaza Afrika Mashariki katika ramani ya soka la Afrika