Match Day : Kaizer Chiefs vs Simba, CAFCL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 May 2021
Match Day : Kaizer Chiefs vs Simba, CAFCL

Saa 12 jioni pale Afrika Kusini ambapo huku Tanzania itakuwa saa moja jioni, Machampioni wa Taifa hili Simba watakuwa dimba la Soccer City (FNB) kuziumiza nyasi katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs

Huu ni mchezo wa kwanza baina ya timu hizi katika historia ya soka la Afrika, hivyo matokeo yoyote yatakayopatikana yataingia katika historia ya vilabu hivi vinavyoongoza kwa idadi ya mashabiki katika nchi zao

Simba imekuwa na msimu mzuri sana katika michuano ya ligi ya mabingwa, ni kama mabingwa hawa wa nchi wameshakula robo tatu ya n'gombe, wamebakisha robo tu ili wakamilishe jambo kubwa la kihistoria

Hivyo ni mchezo ambao Simba haipaswi kupoteza, naamini hata saikolojia za wachezaji ziko hivyo, hakuna anayefikiria kufungwa Afrika Kusini

Ukivitazama vikosi vya timu zote mbili, utakubali kuwa Simba ni bora zaidi ya Chiefs, wajukuu hawa wa Mandela wanapita kwenye kipindi kigumu sana

Jana mashabiki wa timu hiyo waliandamana wakionyesa hasira zao kutokana na kiwango kisichoridhisha cha timu yao kwenye ligi

Chiefs wanashika nafasi ya 10 ambapo katika michezo 12 iliyopita, wameshinda michezo miwili tu

Hata hivyo hautakuwa mchezo wa 'kumsukuma mlevi' kwa Simba kama wengi wanavyodhani

Mara nyingi mechi za aina hii zimetoa matokeo ya kustaajabisha na ndio sababu kocha mkuu wa Simba Didier Gomes amewaelekeza wachezaji wake wacheze kwa nidhamu ya hali ya juu kama walivyofanya katika michezo ya ugenini dhidi ya AS Vita na Al Ahly

Gomes amesema lengo ni kufanya vizuri Afrika Kusini lakini ni muhimu waweke matumaini katika mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es salaam wiki ijayo

"Nimewaambia wachezaji wangu tunapaswa kuwa na nidhamu sana. Hautakuwa mchezo mwepesi, hakuna timu mbovu katika hatua hii tuliyofikia. Tumekuja hapa kusaka matokeo mazuri. Tukipata ushindi ni jambo jema lakini nimewasisitizia lazima tuweke matumaini katika mchezo wetu wa nyumbani," alisema Gomes

Kwa wachezaji wa Simba, kila mmoja alitamani kufika hatua hii. Leo wanacheza katika uwanja wenye historia kubwa. Uwanja ambao mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 ulipigwa, Hispania ikaibuka mabingwa dhidi ya Uholanzi kwa bao la Andres Iniesta

Wachezaji wanafahamu ushindi au hata matokeo ya sare leo, yatawaweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali na kufikia lengo la klabu msimu huu

Gomes amesisitiza kuwa wakivuka hatua hii, watakuwa na haki ya kuzungumzia kushinda ubingwa wa Afrika

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’