Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema wanatarajia mchezo mgumu kutoka kwa Kaizer Chiefs leo katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Hata hivyo amesema lengo lao ni kuhakikisha wanapata ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuingia nusu fainali
Akizungumza katika Mkutano wa Wanahabari kuelekea mchezo huo, Gomes amesema wamekusudia kushinda mchezo huo
"Hii ni Ligi ya Mabingwa, tunatarajia mchezo mgumu kesho hasa sababu tupo ugenini lakini hatutaki kuzuiliwa. Kaizer Chiefs ni timu kubwa hatuwezi kuidharau lakini tupo tayari kupambana," alisema Gomes
Nae nahodha wa Simba John Bocco, amesema wao wachezaji wamejipanga na watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri licha ya kuwa wanatarajia mchezo hautakuwa mwepesi
"Tuko tayari kuipambania timu yetu na kupata matokeo mazuri," amesema
Aidha Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kesho kutakuwa na tuzo maalum ya nyota wa mchezo wa kikosi cha Simba ambapo atakeyeshinda ataondoka na kitita cha Tsh Milioni 2.5