Maandalizi yanaendelea Bondeni, bonus yaongezeka

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 May 2021
Maandalizi yanaendelea Bondeni, bonus yaongezeka

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema walitambua changamoto ya hali ya hewa ndio maana wakawahi kwenda Afrika Kusini kufanya maandalizi ya mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs

Kwa sasa Afrika Kusini ni kipindi cha baridi kali ambapo hali hiyo iliwasumbua kidogo wachezaji katika siku yao ya kwanza

Baada ya kufanya mazoezi kwa siku mbili, Matola amesema wachezaji wameizoea hali hiyo na hivyo wako tayari kwa mchezo wa keshokutwa

"Tunashukuru tunaendelea vyema na maandalizi. Baridi ni kali lakini imekuwa vyema kwetu kwani tumepata muda wa kuzoea, muhimu zaidi tunafanya mazoezi katika muda ambao mchezo utachezwa (saa 12 jioni)"

"Mchezo dhidi ya Chiefs hautakuwa mwepesi kana wengi wanavyouchukulia. Kaizer Chiefs ni timu nzuri inayocheza soka la kasi lakini nasi tunajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo huo," alisema Matola

Naye Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema wao kama viongozi wametimiza wajibu wao kwa kuhakikisha timu inapata kila wanachohitaji kuelekea mchezo huo

"Maandalizi yanakwenda vizuri. Kama viongozi tunazungumza na wachezaji na kuwahamasisha kuhakikisha wanatimiza malengo ya klabu. Kuna mambo mengi tumewaahidi lakini kikubwa ipo bonus kubwa sana kwao kama wataweza kutuvusha katika hatua hii," alisema Barbara

Mchezo dhidi ya Chiefs utapigwa Jumamosi, May 15 katika uwanja wa FNB zamani ukiitwa Soccer City, muda wa mchezo ni saa moja kwa saa za Tanzania

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
8h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’