Tuko vizuri kuwakabili Kaizer Chiefs - Rweyemamu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 May 2021
Tuko vizuri kuwakabili Kaizer Chiefs - Rweyemamu

Meneja wa kikosi cha Simba, Patrick Rweyemamu amesema wako tayari kupambana na kupata pointi tatu kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kazier Chiefs itakaopigwa Jumamosi, May 15 katika uwanja wa FNB

Simba iliwasili Afrika Kusini jana na jioni wachezaji wakapata nafasi ya kufanya mazoezi yao ya kwanza ya maandalizi ya mchezo huo

Rweyemamu amesema timu iliwasili salama, wachezaji wote wana ari, wanaendelea na maandalizi

"Tunashukuru tumefika salama, tunaendelea na maandalizi ya mchezo, muhimu ni kuhakikisha kupata pointi tatu," alisema Rweyemamu

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kati ya Kaizer Chiefs dhidi ya Simba, mabingwa hao wa kihistoria wakipewa nafasi kubwa ya kushinda

Pamoja na kuvuka robo fainali ya ligi ya mabingwa, Chiefs hawana msimu mzuri, katika msimamo wa ligi kuu ya Afrika Kusini, wanashika nafasi ya tisa

Licha ya kuonekana hawako vizuri kwenye ligi, Simba wasiwachukulie kirahisi kwani timu hiyo imepata matokeo katika mechi zenye ushindani ikiwemo kuwafunga mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns kwenye mchezo uliopigwa hivi karibuni

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
2h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
2h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
8h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
1d ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’