Nahodha wa Simba John Bocco amesema wanahitaji kufanya vyema katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa Jumamosi, May 15 huko Afrika Kusini ili kurahisisha kazi ya mchezo wa marudiano ambao utapigwa jijini Dar es salaam May 22
Akizungumza muda mfupi kabla ya timu kuelekea Afrika Kusini mapema leo, Bocco alisema watapambana kuhakikisha wanapata matokeo katika mchezo huo wa kwanza
"Tunajua mchezo utakuwa mgumu, tunawaheshimu Kaizer Chiefs ni timu nzuri na inacheza kwao lakini sisi tumejiandaa kufanya vizuri ili mchezo wa marudiano uwe mwepesi kwetu"
"Sisi kama wachezaji tupo tayari na tumefanya maandalizi mazuri, tuna wachezaji wenye ubora na tuna matumaini ya kufanya vizuri ingawa haitakuwa kazi rahisi," alisema Bocco
Simba imeondoka jijini Dar es salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 24, wachezaji waliobaki ni Perfect Chikwende, Said Ndemla na Miraji Athumani huku Bentard Morrison akitarajiwa kuungana na timu huko Afrika Kusini kesho