Jinsi Al Masry ilivyoiponza Simba kwa Stand United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
3 Mar 2018
Jinsi Al Masry ilivyoiponza Simba kwa Stand United
Moja ya hofu aliyokuwa nayo kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre kabla ya mchezo dhidi ya Stand United leo ilikuwa wachezaji kufikiri zaidi mchezo ujao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry unaopigwa Jumatano ijayo, March 07.

Lechantre alitumia muda mwingi akiwa na wachezaji wake kuwapa hamasa kabla ya mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Kwa mara ya kwanza Simba iliyokuwa na ukuta mgumu kuliko timu zote zinazoshiriki VPL imeruhusu mabao matatu kwenye mchezo mmoja.

Mabao yote yalisababishwa na uzembe katika kukaba. Kitendo cha kuwaruhusu Stand United kurudisha mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza kiliwafanya wazidi kujiamini

Ni dhahiri yale aliyoyasema Lechantre ndiyo yaliyokuwa kichwani kwa wachezaji wa Simba kwani ni kama baadhi yao hawakuwepo uwanjani.

Aina ya makosa yaliyopelekea mabao hayo sio makosa ambayo hufanywa na wachezaji wa Simba wakiwa katika ubora wao.

Kabla ya mchezo wa leo Lechantre aliseme;

“Wachezaji wanafikiria sana kuhusu mechi ya Al Masry hivyo inamaana hawafikirii ligi kuu na hawafikiri kuwa tuna mchezo wa ligi kuu siku ya Ijumaa na ninaogopa kwani wakati mwingine kama hatujajiandaa kupambana siku ya Ijumaa tutakuwa na matokeo mabaya ndiyo maana nimekuwa karibu na wachezaji kwa sababu nataka hamasa kubwa kwenye mchezo wa Ijumaa.”
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1m ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →