Serikali imeiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa kwa Watanzania juu ya hatma ya mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga ambao uliahirishwa juzi baada ya kutokea mkanganyiko wa muda
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa ametoa kauli ya Serikali bungeni leo kuhusu tukio la kuahirishwa kwa mchezo huo uliokuwa uchezwe Jumamosi, tarehe 8/05/2021
Mh Majaliwa ameagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa haraka kwa Watanzania juu ya tarehe ya kuchezwa kwa mchezo huo na pia ieleze utaratibu kuhusu hatima ya waliolipa viingilio ili kushuhudia mchezo huo.
Aidha, Waziri Mkuu amewasihi Watanzania kuwa wavumulivu ili kuipa muda Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia mpira wa miguu ikiwemo TFF kuja na taarifa juu ya hatima ya mchezo huo