Mashabiki waliumizwa, tunawaomba radhi - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 May 2021
Mashabiki waliumizwa, tunawaomba radhi - Manara

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba, Haji Manara amewaomba radhi mashabiki waliojitokeza kwa wingi juzi kushuhudia mchezo dhidi ya Yanga ambao hata hivyo haukufanyika baada ya Yanga kugomea kuingiza timu uwanjani saa moja jioni baada ya mabadiliko ya muda wa mchezo yaliyofanywa na Bodi ya Ligi kwa maelekezo ya Serikali

Kama ilivyo kawaida yake, Manara alifanya kazi kubwa ya kuutangaza mchezo huo katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii

Mwenyewe ameeleza kujisikia vibaya kwani kazi yake kubwa aliyoifanya kwa namna moja au nyingine imekuwa sehemu ya machungu ya mashabiki wengi waliojitokeza uwanjani kuishangilia Simba

"Kuanzia Jumatatu hii nilizunguka kwenye vituo vya redio, televisheni na magazeti kufanya promotion kubwa kuelekea mchezo wa jana (juzi) ambao ulikuja kuahirishwa baadae"

"Sijilaumu kwa kile nilichofanya kwa niaba ya klabu yangu,,lakini nimeumizwa sana kuona Washabiki wake hawakupata walichokitarajia"

"Najihisi ni mkosaji na nadhani kuna haja ya kuwajibika kwa kitendo kile,nilitumia nguvu kubwa kuhakikisha tunajaza uwanja,lakini matokeo yake ni maumivu yaliyoacha doa kuu"

"Nawaza Kwa hisia, kwa nini sauti yangu iwe sehemu ya kuwapa maumivu wengine? Wangapi wamejeruhiwa kimwili ná kiaikili kwa kilichotokea jana? Naogopa na naomba msamaha sana Kwa Washabiki wote hususan mliokuja Kwa Mkapa"

"Binafsi nipo katika kipindi kigumu mno, kila nikiwafikiria washabiki wale ambao wakati wote ndio huufanya mchezo huu wa soka kuwa hivi ulivyo sasa

"Inawezekana nisiwe nahusika hata kidogo kuahirishwa Kwa mchezo ule, lakini nitakuwa mpuuzi nisiposema samahani kwenu,"  aliandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Aidha klabu ya Simba ilitoa taarifa kulaani kuahirishwa mchezo huo huku ikitaka klabu ya Yanga iadhibiwe vikali kwa kutotii maagizo ya TFF na Serikali

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’