Baada ya kuahirishwa mchezo dhidi ya watani Yanga, mabingwa wa nchi Simba wanatarajiwa kuondoka Alfajiri ya kuamkia kesho Jumanne kuelekea Afrika Kusini tayari kwa mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, May 15 uwanja wa FNB huko Afrika Kusini, muda wa mchezo ukitarajiwa kuwa saa moja kamili usiku
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes alieleza masikitiko yake baada ya mchezo dhidi ya Yanga kuahirishwa lakini amesema sasa wameelekeza nguvu zao kwa mchezo dhidi Kaizer Chiefs ambao wanahitaji kupata ushindi ili kutinga nusu fainali
Gomes alitaka kuutumia mchezo dhidi ya Yanga kama sehemu ya maandalizi ya kikosi chake kabla ya kuwakabili Kaizer Chiefs huko kwao
"Tunakabiliwa na mchezo wa ushindani dhidi ya Chiefs, si rahisi mchezo dhidi ya Yanga ilikuwa ni moja ya maandalizi yetu kuelekea mechi hiyo ya michuano ya kimataifa ambayo tunatarajia kuanzia ugenini"
"Ni mchezo muhimu, wachezaji wanajua umuhimu wa mchezo huo hivyo tunahitaji kwenda kutafuta matokeo chanya ili kuendelea kujiimarisha kwenye safari yetu ya Ligi ya Mabingwa Afrika," alisema Gomes.