Vinara wa ligi kuu ya Vodacom, Simba leo wameangusha alama mbili kwenye uwanja wa Taifa baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Stand United katika mchezo mkali wa ligi kuu ya Vodacom.
Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na kutawala dakika 30 za mwanzo vilevile ikafanikiwa kufunga mabao mawili kwenye kipindi hicho.
Beki wa kushoto Asante Kwasi aliifungia Simba bao la kuongoza kwenye dakika ya 6 tu akimalizia kwa urahisi mpira uliokuwa umetemwa na mlinda lango wa Stand kufuatia shuti la Laudirt Mavugo ndani ya 18.

Simba ilipachika bao la pili kwenye dakika ya 23 mfungaji akiwa Laudirt Mavugo aliyeunganisha pasi murua ya Shomari Kapombe aliyewatoka walinzi wa Stand United winga ya kulia.
Baada ya kufunga mabao hayo, wachezaji wa Simba walipunguza kasi waliyoanza nayo hivyo kuwapa nafasi Stand United kuwashambulia.
Tariq Seif aliifungia Stand United bao la kwanza kwenye dakika ya 36 akiunganisha vyema krosi ya Lulambo aliyejaza majaro kutoka winga ya kulia.
Walinzi wa kati wa Simba pamoja na mlinda lango Aishi Manula walijisahau na kumruhusu Tariq atokee nyuma na kuujaza mpira kimiani kwa kichwa.
Simba ikajikuta inaruhusu bao la pili kwenye dakika ya 41 baada ya mpira wa kona uliochongwa na Lulambo kutumbukia moja kwa moja kimiani.
Makosa yaliyofanywa na mlinda lango Aishi Manula kuchelewa kuutokea mpira huo alijikuta akiusindikiza wavuni.

Kipindi cha pili Simba iliingia ikiwa na shauku ya kusaka bao la tatu na ilifanikiwa kutumbukiza wavuni bao hilo kupitia kwa Nicolas Gyan kwenye dakika ya 61
Lakini makosa katika safu ya ulinzi ya Simba yalipelekea tena Stand United kusawazisha bao hilo kupitia kwa Bigirimana Blaise kwenye dakika ya 66.
Licha ya mashambulizi ya hapa na pale kutoka kwa kila upande, mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao 3-3 na kuzifanya timu zote zigawane alama moja moja.
Simba ilicheza bila washambuliaji wake tegemeo John Bocco na Emanuel Okwi ambao licha ya kupona majeruhi yao, walipumzishwa kwa ajili ya mchezo ujao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry utakaopigwa Jumatano, wiki ijayo March 07.
Kukosekana kwa washambuliaji hao kuliilazimu Simba iwatumie Laudirt Mavugo na Nicolas Gyan.
Mavugo alitolewa wakati wa mapumziko ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Juma Liuzio.
Simba inaendelea kubaki kileleni baada ya kufikisha alama 46 ikifuatiwa na Yanga yenye alama 40. Yanga ina mchezo mmoja mkononi pia.
Stand United imepanda hadi nafasi ya nane baada ya kufikisha alama 21.

ADVERTISE HERE