Kwanza tunawapa pole mashabiki wa Simba waliosafiri kutoka Kitwe nchini Zambia hapo jana kwa ajili ya kuinga mkono Simba kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga
Hakika ilikuwa bahati mbaya sana kwao, kwa mchezo kutokuchezwa
Ni vyema TFF wanaangalia uwezekano wa mashabiki kurudishiwa fedha zao baada ya mchezo huo kuahirishwa
Lakini kwa hakika imedhihirisha kuwa Simba sasa imeanza kujiongezea mashabiki wengi kutoka nje ya nchi
Usajili wa wachezaji kutoka Mataifa mbalimbali ambao wanafanya vizuri, wanasaidia kuitangaza Simba katika nchi zao pamoja na mafanikio ambayo Simba inapata katika michuano ya Kimataifa
Mchezo wa jana ulitarajiwa kutizamwa na mashabiki sehemu kubwa ya bara la Afrika
Simba imekuwa gumzo Afrika, wengi wamekuwa na shauku ya kuifuatilia hasa baada ya kuwagaragaza vigogo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wakiibuka vinara wa kundi A katika hatua ya makundi mbele ya Al Ahly na AS Vita