Baada ya kuahirishwa mchezo dhidi ya Yanga, mabingwa wa nchi Simba hawana muda wa kupoteza, wanaendelea na maandalizi ya mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa Ijumaa, May 14 katika uwanja wa FNB huko Afrika Kusini
Aidha kulingana na ratiba, kama hakutakuwa na mabadiliko, keshokutwa May 11 wababe hao wa soka nchini, watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Coastal Union huu ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs kule Afrika Kusini, Simba itarejea nchini kujiandaa na mchezo wa marudiano lakini kabla ya mchezo huo May 19 wanaweza kushuka uwanja wa Mkapa kuikabili KMC
Marudiano dhidi ya Chiefs ni May 22, wiki inayofuata May 29 Simba watashuka uwanja wa Uhuru kuikabili Ruvu Shooting