Manara ataka uchunguzi kuahirishwa kwa mchezo dhidi ya Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 May 2021
Manara ataka uchunguzi kuahirishwa kwa mchezo dhidi ya Yanga

Msemaji na Afisa Habari wa klabu ya Simba amesema kuna ulazima wa kufanyika uchunguzi wa nini kilichosababisha kubadilishwa muda wa mchezo dhidi ya Yanga leo na baadae mchezo huo kuahirishwa baada ya Yanga kuingia mitini

Manara amesema kwa namna yake uchunguzi huo unaweza kulihusisha Bunge la nchi

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Manara ametoa maoni yake kuhusu kadhia hiyo ambayo kwa hakika imetia doa taswira ya soka la Tanzania ambalo kipindi cha karibuni limetizamwa kwa jicho tofauti baada ya mafanikio ya Simba kwenye michuano ya ligi ya mabingwa;

"Kabla ya jambo lolote lile kuendelea iundwe Kamati ya kibunge ijiridhishe kuhusu jambo liliotokea leo,ambalo limeacha maumivu makubwa Kwa Washabiki wa soka nchini zaidi ya elfu arobaini ambao walishalipa viingilio vyao ili kuangalia mechi hyo, lakini pia liliochafua taswira ya nchi kimataifa ukizingatia nchi nyingi za Afrika zilikuwa zimejiandaa kuangalia game hii!!

Baadhi ya hadidu rejea za tume hyo huru ziwe hizi;

Nini kilisababisha mechi hii kusogezwa mbele Kwa masaa mawili?

Why game Yanga na Azam pamoja Yanga na Biashara Mara ambazo nazo zilisogezwa mbele masaa mawili zilichezwa ila hii ya leo imeshindikana kuchezwa?

Uwazi wa kile kilichosababisha mechi isogezwe mbele Kwa masaa mawili na kwa nini Yanga muda mchache baada ya taarifa hiyo kutolewa walitoa taarifa ya kuonyesha kutaka kugomea hiyo mechi?
Je kwa niin ugomeaji huu uwe leo na usiwe katika mechi za Azam au Biashara?

Na kama Serikali ilikuwa na sababu za msingi za kusogeza mbele muda wa mechi Kisha kuiarifu TFF (@tanfootball) na Shirikisho hilo kuviandikia vilabu vyote barua,,Kwa nini Yanga pekee wagomee? Na kama wamegomea why Simba haikupewa ushindi?

Je hakukuwa na mbinu ya makusudi ya kuhairisha hii mechi?. Kama ilikuwepo nini kitaendelea?

Nani atalipa gharama ambazo klabu zimeingia kujiandaa na mechi hii na nani atalipia gharama za Watanzania waliolipa viingilio vyao sambamba na gharama kwa wale waliotoka nje ya Dar?

Hil jambo lisichukuliwe kirahisi rahisi maana limeacha maswali mengi ambayo Watanzania waliolipa viingilio vyao na wale walionunua vifurushi vya @azamtvtz wanapaswa kujua, lakini pia limeitia doa ligi yetu ambayo kwenye siku za Karibuni imekuwa maarufu kote barani Afrika.

@bunge.tanzania la watu linao wajibu wa kusimamia kero za watu kama hz za leo. Ni wao pekee kwa sasa wanaweza kuja na majawabu sahihi juu ya kadhia hii iliyowaumiza Watanzania wengi"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’