Kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hakuna mchezaji ataruhidiwa kucheza bila kuwa na Bima.
Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia jana wakati wa ufunguzi wa semina ya utawala bora kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika katika hoteli ya Rombo Green View, Shekilango mjini Dar es Salaam ambayo ilihusisha klabu zote, zikiwemo kongwe za Simba na Yanga.
Semina hiyo iliandaliwa na Kampuni ya Maendeleo na Utafiti wa Michezo (ISDI) kwa kushirikiana na Alliance Life Asuarance na TFF kwa lengo la kutoa elimu kwa viongozi wa klabu kujua jinsi ya utawala, kujiongoza na kutafuta wadhamini.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo Tumain Katunzi amesema wameamua kufanya semina hiyo kla viongozi wa klabu zinazoshiriki ligi zilizo chini ya shirikisho la soka nchini, baada ya kufanya utafiti na kubaini baadhi ya changamoto ambazo zimekua kikwazo katika maendeleo.
Bin Zubeiry

ADVERTISE HERE