Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amewataka waamuzi wa mchezo wa Jumamosi kati ya Simba dhidi ya Yanga kutenda haki kwa kuzingatia sheria 17 za mpira wa miguu
Manara amesema kutokana na ubora wa Simba, baadhi ya timu zimekuwa na kasumba ya kukamia mechi kwa lengo la kutaka kuwaumiza wachezaji wa Simba
Bosi huyo wa kitengo cha Habari,amesema hatarajii kuona mpira wa rafu na kugongana siku ya Jumamosi
"Tunajua hawatakuja kistaarabu kwa sababu wanafahamu hawana ubavu wa kushindana na sisi. Tunawaomba waamuzi wazingatie sheria 17 kwa kuchezesha kwa haki. Akifanya kosa mchezaji wa Simba aadhibiwe lakini pia hata akifanya wa Yanga aadhibiwe"
"Wasitumie ubovu wa kikosi chao kuja na mbinu y kutaka kuwaumiza wachezaji wetu wakiamini ndio njia inayoweza kutuzuia tusiwafunge," alisema Manara
Mara nyingi Yanga wamekuwa wakitumia nguvu za ziada kila wanapokutana na Simba. Jumamosi waamuzi wanapaswa kuzingatia sheria 17 za mpira wa miguu ili kuhakikisha mchezo huo hauchezwi nje ya taratibu za soka
Baada ya mchezo huo, Simba inakabiliwa na mchezo muhimu wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa kati ya May 14/15 Afrika Kusini
Kabla ya mchezo huo Simba itacheza na Coastal Union uwanja wa Benjamin Mkapa