CAF yafanya mabadiliko ya kanuni ligi ya mabingwa, Shirikisho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 May 2021
CAF yafanya mabadiliko ya kanuni ligi ya mabingwa, Shirikisho

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeongeza idadi ya wachezaji wa akiba watakaokaa katika benchi kutoka 7 hadi 9 kuanzia hatua ya robo Fainali itakayochezwa kuanzia tarehe 14 mwezi huu.

Aidha,  kuhusiana na idadi ya wachezaji watakaoingia ndani kutokea benchi kwenye mechi moja, CAF imesema vilabu vitapewa taarifa hivi karibuni baada ya marekebisho yanayotarajiwa kufanywa na FIFA kupitiwa na IFAB (International Football Association Board) ambao wanahusika na marekebisho ya sheria na kanuni.

Pia Mashirikisho na vyama vya soka vya nchi mbalimbali vitapewa taarifa kuviambia vilabu vitakavyoshiriki Mashindano yajayo ya CAF kwa msimu wa 2021-22, Kwamba wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa Kamati ya Mashindano ya CAF kupitia CMS (Competition Management System) na isiwe zaidi ya tarehe 30 Juni, 2021

Kuhusu usajili wa wachezaji, CAF imesema mwisho ni Julai 10 bila faini. Kipindi cha pili ni kati ya Julai 11 na Julai 20 kwa faini ya Dola za Marekani 250 (Usd 250) kwa mchezaji mmoja

Aidha kipindi cha tatu ni kuanzia Julai 21 hadi Julai 31 ambapo Vyama vya soka haviruhusiwi kuondoa jina la mchezaji yoyote bali kuongeza mpya huku faini ikiwa Usd 500 kwa mchezaji mmoja na hawa wataanza kutumika katika hatua ya pili ya raundi za mwanzo na kuendelea

CAF imesema katika msimu Ujao wa 2021-22, Kocha mkuu lazima awe na Leseni A ya CAF au Pro-License, huku Kocha msaidizi lazima awe na Leseni B ya CAF na kuendelea

Hii ni kwa mashindano yote yani Kombe la Shirikisho na Klabu bingwa.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
31m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’