Mabingwa wa nchi Simba wanaendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumamosi, May 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kocha Mkuu Didier Gomes ana kila sababu ya kushinda mchezo huo, wachezaji wote wako tayari kutumika katika mchezo huo wa dabi ya Kariakoo
Taarifa iliyotolewa na Simba jana, imebainisha kuwa hakuna mchezaji majeruhi, wachezaji wote wako timamu kiafya
"Kikosi chetu leo jioni (jana) kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya watani wa jadi Yanga, utakaopigwa Jumamosi Mei 8, mwaka huu. Mazoezi kuelekea mchezo huo yalianza jana huku wachezaji wote wakishiriki na wakiwa katika hali nzuri. Katika mechi hiyo pia hakuna nchezaji ambaye anatarajiwa kukosekana," ilisema taarifa ya Simba