Sifa kubwa ya Simba na mashabiki wake ni kuteka shoo zinapokuja zile mechi kubwa iwe dabi au Kimataifa
Ni wazi, wakati huu ambao Simba inafanya vizuri Kimataifa tena ikiwa tayari imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi, hakuna Mwanamsimbazi ambaye atakubali kubaki nyumbani
Kuelekea pambano dhidi ya Yanga Mei 8, 2021, uongozi wa Simba umejipanga kujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa mapemaa

Mwenendo wa Simba wakati huu unatisha! Kwa shabiki wa Yanga atahitaji kuwa na moyo kwelikweli kwenda uwanjani siku hiyo kwani uwezekano wa kupata aibu ya mwaka ni mkubwa
Afisa Habari na Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amesema kama ilivyo kawaida, siku hiyo Simba itadhihirisha kuwa ndio klabu pendwa zaidi Tanzania kwa sasa na watahakikisha wanawapa furaha mashabiki watakaojitokeza kwa wingi