Onyango ana jambo lake Jumamosi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 May 2021
Onyango ana jambo lake Jumamosi

Katika mchezo wa duru ya kwanza dhidi ya Yanga, mlinzi Joash Onyango ndiye aliyekuwa shujaa wa Simba akifunga bao la kusawazisha kwenye dakika ya 87 na kuihakikishia Simba kuondoka na alama moja muhimu katika mchezo ambao wengi hawaamini ilikuwaje mnyama hakuondoka na alama zote tatu

Jumamosi ya wiki hii, saa 11 jioni Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo wa pili dhidi ya Yanga kwenye ligi msimu huu

Onyango amewahamasisha mashabiki kuhakikisha wanafurika kwa wingi pale kwa Mkapa kushuhudia buruani ambapo ameahidi safari hii watahakikisha wanaondoka na alama zote tatu

Beki huyo raia wa Kenya amesema mashabiki wa Simba wamekuwa sehemu ya mafanikio wanayopata kutokana na hamasa yao kubwa wanayoipa timu

"Ni mchezo muhimu sana kwetu tunahitaji ushindi ili kuendelea kuongoza ligi lengo likiwa kushinda ubingwa. Mashabiki waje kwa wingi, hamasa yao ni muhimu sana kwetu. Tutahakikisha wanafurahia matokeo mazuri baada ya mchezo kumalizika," alisema Onyango

Onyango alitua Simba mwezi August mwaka jana akitokea klabu ya Gor Mahia ya Kenya. Wakati anatua wapo waliombeza kuwa umri umemtupa mkono lakini kiwango bora alichoonyesha mpaka sasa, watu hao wamepoteana

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’