Manara asisitiza marefa wanawajibika kuwalinda wachezaji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Mar 2018
Manara asisitiza marefa wanawajibika kuwalinda wachezaji
Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amelitaka Shirikisho la Soka nchini (TFF), kusaidia kuwalinda wachezaji.

Haji Manara amesema inabidi TFF wawe makini na wachezaji ambao wamekuwa wakicheza michezo mibaya inayopelekea kuumiza na kumfanya mchezaji awe majeruhi.

Manara ameeleza si kwamba hawataki kupambana mchezoni, la hasha, bali waamuzi wasiruhusu faulo za ajabu zitajazopelekea kuhatarisha hali za kiafya kwa wachezaji ambao ni muhimu vikosini.

"Ni vema shirikisho likasaidia kulinda hawa wachezaji kupitia waamunzi, maana kumekuwa na rafu nyingi za ajabu ambazo zinapelekea kuwakosa wachezaji muhimu kikosini, tunakubali mchezo wa mapambano, lakini si faulo ambazo hazina maana" amesema Manara.

Hivi karibuni Simba imemkosa mchezaji wake John Bocco katika mechi mbili zilizopita baada ya kumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC.

Vilevile Emmanuel Okwi naye aliumia katika mchezo uliopita kwa kuchezewa rafu walipokutana na Mbao FC ya jijini Mwanza.

Wawili hao huenda wakaukosa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Stand United leo. Simba inakabiliwa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry Jumatano ijayo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
2h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
21h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
2d ago
READ MORE β†’