Mashabiki wamtaka Morrison mechi ya Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 May 2021
Mashabiki wamtaka Morrison mechi ya Yanga

Jumamosi ijayo moto utawaka pale uwanja wa Benjamin Mkapa wakati mabingwa wa nchi Simba watakaposhuka dimbani kuwakabili watani zao Yanga katika mchezo wa duru la pili, ligi kuu ya Vodacom

Jana 'Lunyasi' walikuwa hapo kwa Mkapa kugawa dozi kwa Kagera Sugar, wakiondoka na ushindi wa mabao 2-1 na kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam

Jina la winga Bernard Morrison lilitajwa sana baada ya mchezo huo kutokana na kazi nzuri aliyofanya

Simba ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0. Lakini alipoingia Morrison katika kipindi cha pili, akafanya kazi yake vyema akifunga bao moja na kutengeneza la pili

Mikimbio yake iliwapa wakati mgumu Kagera Sugar waliokuwa wanajilinda kwa muda wote wa kipindi cha pili kujinusuru na kipigo cha mbwa koko kutokana na msako mkali uliokuwa ukifanywa na Simba

Bahati mbaya kocha Didier Gomes amekuwa akimtumia Morrison akitokea 'sub' lakini kama angekuwa akimuanzisha pengine Simba ingekuwa ikinufaika zaidi na uwepo wake

Pengine ndio sababu mashabiki wanataka kumuona Morrison akianza katika mchezo ujao dhidi ya waajiri wake wa zamani, Yanga

Morrison aliifunga Simba wakati alipokuwa Yanga pengine hii ni nafasi yake kuwalipa Wanamsimbazi kwa kulirejesha bao lile alilofunga Machi 08 2020

"Morrison alibadili mchezo kwenye kipindi cha pili, ana kasi na mara nyingi anapopata mpira yeye hutizama mbele tu. Haijalishi Simba imefunga mabao mangapi, yeye anapokuwa uwanjani anafikiria kufunga au kutengeneza nafasi ili wenzake wafunge. Nadhani kocha anapaswa kumuanzisha kwenye mchezo dhidi ya Yanga Jumamosi," alisema shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Sayeed

Katika mchezo wa duru ya kwanza uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 Morrison hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo huo

Lakini hakuna shaka Jumamosi watakutana nae pale kwa Mkapa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’