Ni kawaida hapo uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Simba kushinda. Ni ushindi mwingine wa mabao 2-1 ambao Simba wamepata dhidi ya Kagera Sugar na kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Simba iliuanza mchezo huo taratibu na haikushangaza kuwashuhudia mabingwa hao wa nchi kuwa nyuma kwa bao 1-0 mpaka wakati wa mapumziko
Kipindi cha pili kilikuwa cha Bernard Morrison ambaye ndiye aliyeamua matokeo ya mchezo huo

Aliisawazishia Simba akimalizia krosi ya Luis Miquissone kabla ya kutengeneza bao la pili lililowekwa kambani na Meddie Kagere ambaye hata hivyo hakumaliza mchezo baada ya kupata majeraha
Kipindi cha pili Simba walikuwa bora na walicheza vile ambavyo mashabiki wamezoea kuwaona
Wametinga hatua ya robo fainali sasa wakisubiri droo ya hatua hiyo mpango ukiwa kutetea taji la FA walilotwaa msimu uliopita
Machampioni wanajiandaa na mchezo dhidi ya watani zao Yanga ambao utapigwa May 08
Hawataamini siku hiyo....!