Tumejipanga kufika mbali zaidi - Gomes

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 May 2021
Tumejipanga kufika mbali zaidi - Gomes

Baada ya Simba kupangwa na Kaizer Chiefs katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema wako tayari kuwakabili Kaizer Chiefs wakiwa na malengo ya kufika mbali zaidi katika michuano ya msimu huu

Gomes amesema Simba imelenga kuvuka hatua ya robo fainali hivyo wamejipanga kucheza vizuri kusaka matokeo yatakayowapeleka nusu fainali

"Tunataka kufika mbali kwenye mashindano haya na tupo tayari kucheza vizuri dhidi ya Kaizer Chiefs kwenye michezo yote. Haitakuwa rahisi lakini nina uhakika huu msimu Simba inaweza kwenda mbali zaidi," alisema Gomes

Mchezo wa kwanza utapigwa Afrika Kusini kati ya May 14/15 wakati mchezo wa marudiano utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa wiki moja baadae

Hii ni nafasi kwa Simba kuandika historia mpya ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika kwa ngazi ya vilabu

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’