Majira ya saa tisa Alasiri leo Ijumaa, April 30 2021 droo ya hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kombe la Shirikisho itafanyika nchini Misri
Mabngwa wa Tanzania Simba Sc ni miongoni mwa timu nane ambazo zinazubiri kufahamu wapinzani wao katika hatua ya robo fainali
Simba ilitinga robo fainali ikiongoza kundi A baada ya kujikusanyia alama 13
Katika droo hiyo hawatapangwa na vinara wengine wa kundi pamoja na Al Ahly iliyomaliza nafasi ya pili nyuma ya Simba kundi A
Kati ya Kaizer Chiefs (Afrika Kusini), MC Alger (Algeria) na CR Belouizdad (Algeria) moja itapangwa na Simba
Hizi ni timu zilizomaliza katika nafasi ya pili kundi B, C na D
Mnyama yuko tayari kukutana na yeyote kati yao na habari njema ni kuwa mchezo wa kwanza utapigwa ugenini na kuja kumaliza kazi jijini Dar es salaam