Kwa mujibu wa takwimu za viwango zilizotolewa na Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) leo, mabingwa wa nchi Simba wamepanda kwa nafasi 15 kutoka nafasi ya 28 waliyokuwepo msimu uliopita na sasa wako nafasi ya 13
Takwimu hizo zimetolewa siku moja kabla ya droo ya hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa na ile ya kombe la Shirikisho
Droo hiyo itafanyika nchini Misri kesho Ijumaa
Ni suala la muda tu, Simba itatinga 10 bora ya miamba ya soka barani Afrika

ADVERTISE HERE