Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes ameupongeza uongozi wa Simba kwa kuwaongeza mikataba manahodha John Bocco na Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr'
Gomes amesema wachezaji hao ni muhimu katika kikosi chake na amefurahi ataendelea kuwa nao kwa muda mrefu zaidi
"Nina furaha sana sababu ni jambo muhimu kwa Simba kusaini mikataba mipya na Mohamed Hussein na John Bocco. Ni wachezaji muhimu na jambo jema kuendelea kuwa nao. Naamini uwepo wao utatusaidia kufika mbali," alisema Gomes
Bocco na Zimbwe Jr walisaini mikataba mipya ya kuendelea kubaki Msimbazi ambapo Bocco alisaini mkataba wa miaka miwili wakati Zimbwe Jr alimwaga wino kwa mkataba wa miaka mitatu

Simba inaendelea kuhuisha mikataba ya wachezaji wake ambao wamependekezwa na kocha Gomes waendelee kubaki kikosini