Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre ameeleza sababu ya kutoonekana kikosini kwa kiungo mshambuliaji Mohammed Ibrahim 'Mo'.
Lechantre amesema hafurahishwi na tabia ya mchezaji huyo ya kutohudhuria mazoezi mara kwa mara akitoa sababu zisizo na msingi.
Lechantre ameyazungumza hayo leo mbele ya waandishi wa habari waliotaka kujua hatma ya kiungo huyo ambaye hajaonekana kwa muda mrefu katika kikosi cha Simba.
"Siwezi kufanya kazi na wachezaji ambao hawafahamu wajibu wao. Hawajitumi kila siku wanajipa likizo zisizo na msingi," alisema Lechantre.
Mo hajaonekana kwenye kikosi cha Simba tangu Pierre Lechantre alipokabidhiwa majukumu ya kukinoa kikosi cha Simba baada ya kutimuliwa Joseph Omog.

ADVERTISE HERE