Jana Kamati ya Uendeshaji wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB), ilimpa onyo winga Bernard Morrison kwa tukio la kumvuta jezi mwamuzi msaidizi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc
Kamati hiyo iliridhia kadi ya njano aliyopewa baada ya tukio hilo na hivyo hatapewa adhabu zaidi
Hii ni habari mbaya kwa watani kwani walijaribu kila jitihada kuona winga huyo anafungiwa ili akose mchezo wa May 08
Katika hatua nyingine Kamati imemfungia michezo mitatu beki Ibrahim Ame na kumtoza faini ya sh. 500,000 kwa kosa la kumzuia mwamuzi msaidizi kufanya kazi yake wakati wa mchezo dhidi ya Gwambina ulichezwa Jumamosi iliyopita,Mwanza.
Aidha Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kocha la mashabiki wake kurusha chupa uwanjani na kusababisha mchezo kusimama dakika tatu hadi Polisi kuingilia kati wakati timu hiyo ilipocheza na Gwambina.
Pia mwamuzi wa mchezo huo, Godfrey Msakila, ameondolewa katika ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu kutokana na kushindwa kumudu mchezo