Mnyama ameunguruma uwanja wa Benjamin Mkapa akiwachabanga watoto wa Makao Makuu, Dodoma Jiji mabao 3-1
Dodoma Jiji 'walikaza' mpaka wakati wa mapumziko wakiwa nguvu sawa na Simba timu zote zikiwa zimefungana bao 1-1
Chris Mugalu aliitanguliza Simba kwa bao safi kabla ya Cleofas Mkandala kuisawazishia Dodoma Jiji
Kipindi cha pili Simba ilirejea ikiwa imara na kuongeza umakini waliokuwa wameukosa kwenye kipindi cha kwanza
Luis Miquissone na Chris Mugalu wakafunga mabao mengine mawili yaliyoihakikishia Simba kujichimbia kileleni kwa tofauti ya alama nne baada ya kufikisha alama 61
Mugalu amefikisha mabao nane wakati Miquisone amefunga bao lake la saba leo
Kesho Simba itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mbeya Kwanza mchezo ukitarajiwa kupigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Mchezo utakaofuata ni kombe la FA dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa May 01, hapo machinjioni kwa Mkapa
May 08 tena Mnyama atarejea hapo kwa Mkapa kuwaadhibu watani zake Yanga