Mashabiki wameaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuiunga mkono Simba katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa kuanzia saa moja usiku
Ukiwa shabiki wa Simba hupaswi kukosa mechi hizi kwani jambo moja la uhakika ni kuwa upata burudani kwa asilimia 100
Baada ya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi, Mnyama leo amepania kuwapa mashabiki wake burudani ya kibingwa kwani wana uhakika hawatatoka tena katika nafasi hiyo
Huu ni mchezo ambao utarajie kukishuhudia kile kikosi cha maangamizi kilichowatesa vigogo huko kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Kocha Didier Gomes amedhihirisha kuwa hana 'shughuli ndogo' na hana kawaida ya kudharau mechi
Ni mwendo wa vipigo kwa kila anayekuja mbele iwe ligi au kule kwenye michuano ya ligi ya mabingwa