Ni mwendo wa kukusanya alama tatu kila mchezo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Apr 2021
Ni mwendo wa kukusanya alama tatu kila mchezo

Baada ya kushinda michezo yote mitatu kanda ya ziwa na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi, kocha mkuu wa Simba Didier Gomes amesema wamedhamiria kushinda kile mchezo ujao ili kuhakikisha wanatetea ubingwa walioshinda kwa misimu mitatu mfululizo

Simba leo jioni itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kuanzia saa moja usiku

Gomes amesema baada ya kuwa wamefanikiwa kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi, kazi iliyobaki ni kuhakikisha wanabaki katika nafasi hiyo mpaka mwishoni mwa msimu

"Tumefanikiwa na kutimiza lengo letu kama timu kiu yetu ilikuwa kupanda juu ya msimamo wa ligi jambo ambalo limefanikiwa sasa rasmi tumeanza mbio za kulisaka taji la Ligi Kuu"

"Halikuwa jambo rahisi lakini wachezaji wangu wamepambana na kufanikisha hili tunashiriki mashindano mengi ambayo tunapaswa kupambana kwa nguvu na kulipa fadhila kwa mashabiki wetu ambao wamekuwa wakitusapoti bila kuchoka ," alisema Gomes

Katika mwezi huu April, Gomes ameiongoza Simba kushinda mechi zote nne, mchezo wa leo dhidi ya Dodoma Jiji ukiwa wa tano

Haitashangaza Gomes kupewa tuzo ya kocha bora wa mwezi huu kutokana na mafanikio hayo aliyopata

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’