Mzozo ataka Milioni 100 mezani usajili wa Zimbwe Jr

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Apr 2021
Mzozo ataka Milioni 100 mezani usajili wa Zimbwe Jr

Meneja wa mchezaji Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr', Herry Mzozo amesema watasubiri msimu umalizike ili kujua hatma ya mlinzi huyo mahiri wa kushoto ambaye bado hajaongeza mkataba kuendelea kuitumikia Simba

Mzozo amesema alitegemea baada ya mkataba wake kubakisha miezi sita walipaswa kukaa mezani kukubaliana na kusaini kandarasi mpya lakini jambo hilo halijafanyika mpaka sasa

"Kwa kawaida mchezaji akibakisha miezi sita kama anahitajika klabuni lazima mkae mezani kujadiliana na kusaini mkataba mpya. Walimtuma mtu akaja tukawa hatujakubaliana lakini alivyoondoka hajarudi tena kwetu," amesema Mzozo

Mzozo amesema tayari amepokea ofa kutoka kwa timu za Mamelod Sundowns na Kaizer Chiefs zote za Afrika Kusini kutaka saini ya mlinzi ya mlinzi huyo

Mzozo ameweka wazi kuwa dau la kumpata Zimbwe Jr kwa timu itakayo muhitaji ni milioni 100 na mshahara wa milioni 8 hadi 10 kwa mwezi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’