Baada ya hapo jana Yanga kuachia mamlaka yote ya ubingwa kwa Machampioni watetezi Simba kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam Fc, wekundu wa Msimbazi wamepania kumaliza kazi May 08 pale kwa Mkapa timu hizo zitakapokutana katika mchezo wa marudiano
Kesho Simba itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuumana na Dodoma Jiji ambapo baada ya mchezo huo, mechi itakayofauata ni dhidi ya Yanga May 08 ingawa May 01 kutakuwa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Kagera Sugar
Msimu uliopita Simba iliifumua Yanga 4-1 katika mchezo wa nusu fainali kombe la FA, Wanamsimbazi wameanza kupigia hesabu kipigo cha aina hiyo
Kwa hakika siku hiyo itabidi 'uto' wajipange kwelikweli maana Mnyama wa sasa sio yule waliyecheza nae mwanzoni mwa msimu
ADVERTISE HERE