Bocco, Okwi warejea mazoezini

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Mar 2018
Bocco, Okwi warejea mazoezini
Mshambuliaji Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi jioni ya leo anatarajiwa kufanya mazoezi baada ya mapumziko ya siku tatu kufuatia maumivu ya kifundo cha mguu.

Okwi aliumia Jumatatu wiki hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC baada ya kugongana na mchezaji wa zamani wa Simba B, Boniphace Maganga na kushindwa kuendelea na mchezo baada ya dakika 80, nafasi yake ikichukuliwa na Mrundi, Laudit Mavugo.

Okwi aliondoka uwanjani akiwa amekwishaifungia Simba mabao mawili, mengine yakifungwa na Shiza Kichuya, Erasto Nyoni na Mghana, Nicholaus Gyan.

Pamoja na Okwi, mshambuliaji mwingine tegemeo wa timu hiyo na Nahodha, John Raphael naye anatarajiwa kuendelea na mazoezi leo baada ya kuanza jana kufuatia mapumziko ya takriban wiki mbili.

Bocco aliumia Februari 15 katika sare ya 2-2 na wenyeji, Mwadui FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na tangu hapo amekosa mechi mbili, marudiano Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gendarmerie Tnare nchini Djibouti, Simba ikishinda 1-0 bao pekee la Okwi na dhidi ya Mbao FC.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’