Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amewapongeza wachezaji kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gwambina Fc na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi
Matola amesema Matokeo hayo yanamaanisha kuwa wameanza rasmi kazi ya kutetea ubingwa wao kwa msimu wa nne mfululizo
Hata hivyo amehoji kukataliwa kwa bao lililofungwa na Joash Onyango, akibainisha kuwa benchi la ufundi watapitia picha za marudio kubaini sababu ya goli hilo kukataliwa
"Baada ya kukaa kileleni sasa ndio kazi imeanza katika harakati zetu za kusaka ubingwa na kuzidi kushiriki kimataifa"
"Lakini licha ya ushindi huu tulioupata hatuelewi sababu ya Mwamuzi kukataa bao letu la pili, tunanda kutazama kwenye TV na kujiridhisha. Vijana niwapongeze kwa sababu leo ni siku yangu ya kuzaliwa wamenipa furaha, tumeingia kileleni na bado tuna vipolo kwahiyo tunachotaka ni kubeba tena Ubingwa," alisema Matola