Mabingwa wa nchi Simba jioni ya leo majira ya saa kumi watashuka katika uwanja wa Gwambina Complex, Misungwi kuwakabili wapinzani wao Gwambina katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Simba imefanikiwa kukusanya alama sita kati ya tisa walizozifuata kanda ya ziwa, leo wanahitaji alama nyingine tatu ambazo ni muhimu sana
Alama hizo tatu zitaishuhudia Simba ikipanda kileleni mwa msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza mwaka 2021 wakiwapiku watani zao Yanga
Huo unaweza kuwa mwanzo wa mashabiki wa Simba kuanza hesabu za siku ya kukabidhiwa ubingwa wa nne kwani Mnyama akikaa pale juu sidhani kama itakuwa rahisi tena kumshusha
Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola aliwaambia wanahabari jana kuwa timu iko tayari kwa mchezo huu, wamedhamiria kuondoka na alama zote tatu licha ya kukabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mfululizo
Katika mchezo huo Simba itamkosa kiungo Taddeo Lwanga ambaye jana alipata msiba wa kufiwa na dada yake
Kila la kheri Simba, kila la kheri mabingwa wa nchi