Kiungo mshambuliaji wa Simba Benard Morrison atakosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa uwanja wa Kaitaba leo akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Morrison alionyeshwa kadi ya tatu katika mchezo uliopita dhidi ya Mwadui Fc baada ya kumvuta mwamuzi jezi katika jitihada za kumuondoa ili apige mpira wa kona
Hata hivyo kukosekana kwake hakuwezi kuwa tatizo kwa mabingwa hao wa nchi kwani wamesheheni wachezaji bora katika kila nafasi
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes leo anatarajiwa kutumia kikosi chake kamili, hasa ikizingatiwa uwanja wa Kaitaba unaruhusu 'pira biriani' kupigwa
ADVERTISE HERE