Mabingwa wa nchi Simba wako mkoani Kagera ambapo jioni ya leo watashuka uwanja wa Kaitaba kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya kushinda mechi zote mbili zilizopita, Simba imepania kuendeleza wimbi la ushindi mkakati uliopo ni kuhakikisha mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi huu wawe kileleni
Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa Kagera Sugar lakini wamejipanga kushinda mchezo huo
Akizungumza na wanahabari jana kuelezea maandalizi ya kikosi chake, Matola alisema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo, hakuna majeruhi
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0
Huu ni mchezo mwingine ambao 'Mnyama' anazihitaji alama zote tatu