Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema timu imewasili salama mkoani Kagera tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Kaitaba
Akizungumzia maandalizi ya kikosi kuelekea mchezo huo, Matola amesema wanatambua ugumu wa mchezo lakini wamejipanga kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu
"Tunashukuru tumesafiri salama tukiwa na karibuni kikosi kizima. Kesho tutacheza mechi ngumu dhidi ya Kagera Sugar. pamoja na kuwa wako chini kwenye msimamo, lakini wana timu nzuri yenye wachezaji wazoefu"
"Hivi karibuni wamebadilisha mwalimu na utaona michezo waliyocheza wamefanya vizuri"
"Jambo jema kwetu sisi tuko kamili, bahati nzuri hatuna mchezaji majeruhi, tutahakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo huo," alisema Matola
Simba ilitua Kagera mchana wa leo wakitokea jijini Mwanza ambako wameweka kambi