Bila Mo tusingekuwa hapa - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Apr 2021
Bila Mo tusingekuwa hapa - Manara

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amesema unazungumzia mafanikio wanayopata Simba sasa nyuma yake yupo Mwekezaji ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bilionea Mohammed Dewji 'Mo'

Leo kitafanyika kikao kati ya Simba, FCC na Serikali ili kupata mwafaka wa sintofahamu iliyojitokeza kati ya Simba na FCC (Tume ya Ushindani) ambayo iliiagiza klabu ya Simba kuanza upya mchakato wa Mabadiliko

Wadau wengi wa soka wakiwemo wabunge kule mkoani Dodoma walionyesha wasiwasi wao kuwa FCC hawaitendei haki Simba ambayo tayari imepiga hatua kubwa katika mchakato wake

Manara amesema Mo anapaswa kuungwa mkono katika jitihada zake anazozifanya ndani ya klabu ya Simba ambazo pia zinasaidia kukuza soka la Tanzania

"Mo ndio chachu ya mafanikio makubwa ambayo Simba imepata katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu"

"Unapoizungumzia Simba sasa, unazungumzia moja ya klabu nane bora barani Afrika wakati huu"

"Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,kusema ukweli bila Mohamed Dewji Simba isingekua hapa. Nani angetoa mahela yote yale kumsajili mchezaji kama Miquissone?"

"Mishahara peke yake ndani ya Simba ni zaidi ya Milioni 300 kwa Mwezi. Ni kama Wizara, yaani ni dude Moja kubwaaaaa," alisema Manara katika mahojiano na Wasafi Fm

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8m ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
15h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
15h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
18h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’