Kocha Mrundi wa Simba, Masoud Djuma hana masikhara kabisa kwani anawanyoosha vilivyo mastaa wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi, Kariakoo.
Djuma ambaye ni kocha msaidizi, alianza kuwanyoosha mastaa wa timu hiyo kwa kuwafanyia mabadiliko ya mapema tu, alipokuwa akikaimu nafasi ya kocha mkuu, siku chache baada ya Simba kusitisha mkataba wa Mkameruni, Joseph Omog.
Wakati Djuma anakaimu nafasi hiyo aliongoza Simba katika mechi tatu ambazo zilikuwa dhidi ya Ndanda, Singida United na Kagera Sugar ambazo zote alishinda lakini lakini kocha huyo amewaonjesha joto ya jiwe mastaa wanne wa maana.
Katika mechi ya Ndanda ambayo Simba walishinda 2-0, ambayo yote yalifungwa na John Bocco alimtoa kiungo Mohammed Ibrahim 'MO' katika dakika 34, na nafasi yake aliingia Said Ndemla.
Djuma ambaye kwa sasa amekuwa na sauti kubwa kwenye benchi la ufundi pamoja na kwamba bosi wake ni Pierre Lechantre raia wa Ufaransa, alifanya hivyo tena kwa kumtoa Jamali Mwambeleko katika dakika 42 walipoifunga Majimaji mabao 4-0.
Katika mechi ya Singida United ambayo walishinda 4-0, Djuma alimfanyia mabadiliko Mwinyi Kazimoto katika dakika ya 22, kipindi cha kwanza na kuingia Said Ndemla.
Kama hiyo haitoshi, kwenye mechi dhidi ya Mbao alifanya hivyo kwa kumtoa Ndemla dakika ya 31 na nafasi yake kuchukuliwa na Ndemla.
Akitolea ufafanuzi sakata hilo, Djuma alisema kwa wachezaji siku hazifanani kwani mpaka mchezaji apate nafasi kikosi cha kwanza, anakuwa amefanya vizuri katika mazoezi lakini anaweza kuingia uwanjani mambo yakabadilika.
"Katika kusaka ushindi kama kuna mchezaji anashindwa kufanya vizuri haina haja ya kumsubiri, dawa ni kumtoa mapema ili aingie mwingine na kufanya kazi kwa ufasaha," alisema.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE