Ni alama tatu nyingine Simba imevuna mkoani Shinyanga baada ya kuichapa Mwadui Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kambarage
Haukuwa mchezo mwepesi sana kutokana na aina ya mbinu waliyotumia Mwadui Fc ambao muda mwingi wakikuwa nyuma ya mpira wakijilinda
Hata hivyo faida ya kuwa na washambuliaji wenye uzoefu imekuwa na manufaa kwa Simba kwani katika dakika ya 66 Bocco aliifungia Simba bao pekee lililowahakikishia alama zote tatu
Hilo lilikuwa bao lake la 10 msimu huu
Ushindi huo unaisogeza Simba kwenye nafasi ya pili ikifikisha alama 52, alama mbili nyuma ya Yanga yenye alama 54
Mpango wa Simba ni kuondoka na alama zote tisa kanda ya ziwa
Alama tatu tayari zimepatikana, alama nyingine sita ziko mikononi mwa Kagera Sugar na Gwambina Fc
Jumatano Simba iitakuwa Kagera kuwavaa Kagera Sugar
Β