Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa jana alikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu Simba Barbara Gonzalez, kujadili mgogoro kati ya timu hiyo na Tume ya Ushindani (Fair Competition Comission, FCC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri, katika mazungumzo hayo, Barbara, amemhakikishia Waziri kushirikiana na tume hiyo ili kumaliza mgogoro huo.
Mazungumzo hayo yamefanyika jana Aprili 15,2021, jijini Dar es Salaam, ambapo Mtendaji Mkuu huyo wa Simba, ameishukuru Serikali kuingilia kati mgogoro huo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kuendeleza soka nchini
ADVERTISE HERE