Kiungo mshambuliaji wa Simba Larry Bwalya amesema ni muda sasa wa Simba kupata mafanikio Kimataifa pamoja na kuendelea kufanya vizuri katika ligi ya ndani
Bwalya amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Simba juzi akifunga moja ya mabao yaliyoihakikishia Simba kuondoka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya kufunga bao, Bwalya alishangilia bao hilo kwa staili ya kuonyesha wakati katika mkono wake
Bwalya amefafanua aina hiyo ya ushangiliaji kuwa alimaanisha kuwa sasa ni wakati wao kutamba Kimataifa pamoja na ligi ya ndani
Ikumbukwe Simba imetinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ikisubiri droo ya hatua hiyo ambayo itapangwa April 30, 2021
"Nilishangilia kwa staili ya kupiga mkononi sababu nilikuwa naonyesha muda wa Simba kufanya vizuri ndani na nje ya nchi umefika," alisema Bwalya
"Simba ni timu kubwa na ipo kwenye kiwango bora sasa ni wakati wa kila mchezaji kuisaidia ili kupiga hatua kwenda mbele zaidi"
Ushindi waliopata Simba dhidi ya Mtibwa Sugar, umewasogeza karibu na kileleni mwa msimamo wa ligi sasa wakitofautiana alama mbili tu na Yanga lakini pia wakiwa na michezo mitatu ya viporo
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Mwadui Fc na utapigwa April 18 kule Shinyanga